Steven Seagal - Huyu wote
tunamkumbuka kwa movie zake za kuvunjana enzi zile za kuangalia movie za
Mkandala, kwa sasa maisha ya movie hayana jipya kwake kwani waigizaji
wapya kama Jet Lee wameshaiteka sanaa.
Macaulay Culkin - Bila
shaka huyu aliikosha mioyo yetu enzi zile tunaanza kuwa wapenzi wa
filamu, movie zake zilizoutikisa ulimwengu kama ‘Home Alone’ zilioneshwa
sana mitaani na kwenye mabasi yaendayo mikoani wakati wa safari. Hivi
sasa hata haieleweki kapotelea wapi.
Demi Moore - Huyu
mwanamama alishawahi kuwa mke wa staa maarufu wa movie za kivita, Bruce
Wills, na baadaye kufunga ndoa na Serengeti Boy, ‘Ashton Kutcher’ kutoka
kwenye kipindi cha ‘Punkd’. Baada ya kuachika kote, hivi sasa bado
hasomeki katika ramani ya filamu, mara ya mwisho kutoa movie ni siku
nyingi zilizopita.
Nicolas Cage - Nani
ataisahau ile movie ya Ghost Rider, yule jamaa anayeendesha pikipiki
huku akifoka moto kichwani. Na ile ya FACE-OFF aliyoigiza na John
Travolta? Huyu siyo mgeni, hivi sasa anasifika kwa kutengeneza movie
zisizofikia kiwango na kumfanya kupuuziwa kwenye gemu.
John Travolta - Ukweli ni
kwamba kilicho juu kisubirie chini, licha ya kuwa na ndege binafsi,
Johnny alianza kufifia baada ya movie yake ya ‘Pulp Fiction’
iliyompunguzia makali ya uigizaji wake na kushushwa kiwango.
Renee Zellweger – Huyu
mwanadada ambaye hajaigiza katika movie yoyote kwa muda wa miaka minne
sasa, alisifika sana kwenye movie na Tom Cruise ya Jerry Maguire na
kuingiza sauti katika katuni ya Shark Tale akiwa na mkongwe Will Smith.
Eddie Murphy – Angetokea
Afrika nahisi angeshakuwa mfalme, movie yake wote tulishaiona, ile ya
kupigishwa mpaka mswaki, Coming to America. Hivi sasa hana movie yoyote
iliyouza viwango vyake vya zamani ukiachana na ile aliyoingiza sauti
kama punda katika katuni maarufu ya Shrek.
Shannen Doherty -
Mwanadada huyu alisifika sana katika TV Series kama Beverly Hills 90210
na Charmed, hivi sasa ana miaka 10 hajatoa kazi yoyote.
Jean-Claude Van Damme -
Huyu jamaa alitukosha sana na mateke yake kwenye movie zake, aliuteka
ulimwengu kipindi cha miaka ya 1980 na 1990 lakini kama ilivyo kawaida
kwa wacheza movie za kupigana, wanavyozidi kuzeeka na wasifu wao huzidi
kufifia.
Mel Gibson - Huyu ndiyo
jamaa aliyeongoza wanajeshi katika movie ya Braveheart na kutengenza
movie kama Apocalipto na Passion Of Christ. Hivi sasa kila mmoja
akijaribu kumsoma atasema huyu jamaa ameshafyatuka akili kwa maneno ya
kibaguzi anayoyatoa. Tabia ya ubaguzi huo ndiyo imekuwa chanzo cha kufa
kwa sanaa yake. Hivi sasa bado hatuelewi anashughulika na nini.
Pauly Shore - Huyu naye
alitamba sana kipindi cha miaka ya 1990 na movie yake ya Encino
iliyompatia umaarufu mkubwa. Hivi sasa bado anaigiza movie mbili tatu
lakini siyo kiwango alichowahi kufikia kipindi chake cha nyuma.
Helen Hunt - Alikimbiza
sana katika kipindi chake cha ‘Mad About You’, akafanya kazi nzuri tena
kama ‘Cast Away’ lakini sasa hatujui mengi kuhusu mwanadada huyu ambaye
hasomeki amekimbilia wapi.
Jerry Seinfeld - Jamaa
alisifika sana katika runinga na kipindi kilichofanya vizuri sana katika
anga za uigizaji lakini sasa anaandika ‘web series’, kitu ambacho kila
mtu anahisi jamaa amefulia kwelikweli.
Sylvester Stallone –
Inatia huruma sana kutoka katika movie ya Rocky hadi kuigiza katika The
Expendables, movie ambayo hufufua waigizaji wa zamani (mababu). Movie
hiyo ya mababu inafanya vizuri lakini katika kiwango cha chini kwani
wahusika wote walishafifia katika anga za filamu.
Meg Ryan- Mwanadada
aliyesifika kwa kufeki mahaba katika filamu ya When Harry Met Sally
mwaka 1989, alishwahi kuwa na movie zilizokimbiza baada ya ile lakini
hivi sasa kipaji na kazi zake zimeshafifia.
0 comments:
Post a Comment