ROJO ATUA MAN UNITED KUKAMILISHA USAJILI


 
Marcos Rojo akiwa na wafanyakazi wa Man Utd katika Hospitali ya Bridgewater baada ya kutua tayari kufanyiwa vipimo.
...Rojo akielekea kufanyiwa vipimo.
Mchezaji wa Argentina, Marcos Rojo akiwa kazini.
  Mshambuliaji wa Man Utd, Luis Nani amejiunga na Spoting Lisbon kwa mkopo.
KLABU ya Manchester United imekubali kutoa pauni milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo.
Rojo, ambaye ametua mjini Manchester jana jioni na kusema kuhamia United ‘anahisi kama ndoto’, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne akifaulu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi vya kandarasi yake.
Louis van Gaal ametoa kipaumbele kwa usajili wa beki huyo mtumia mguu wa kushoto, Rojo, mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England Jumamosi iliyopita  na Swansea.
Winga Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa pauni milioni 17 mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo katika klabu yake hiyo ya zamani, ikiwa ni sehemu ya dili hilo la Rojo.
                                     
                  Posted by MR.Prime on August 20, 2014 
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment